NSSF EMPLOYEES SACCOS

NSSF EMPLOYEES SACCOS LTD

Utawala

Utangulizi

Muundo wa Chama unaojumuisha:- 

  • Mkutano Mkuu,
  • Bodi ya Chama,
  • Kamati mbali mbali,
  • Kamati ya Usimamizi,
  • Meneja,
  • Idara na vitengo vyake

kama itavyofafanuliwa kwenye Sera ya ajira na utumishi.

Vilevile, Chama kinaweza kuongeza watendaji kwa siku zijazo ili kutekeleza mikakati ya Chama kwa wakati.

Mkutano Mkuu

Hiki ndicho chombo kikuu cha maamuzi katika Chama.Wajibu wa Mkutano Mkuu umeelezwa katika Masharti ya Chama katika sehemu ya Tisa. 

Bodi ya Chama

Hiki ndicho chombo kikuu cha usimamizi wa shughuli zote za Chama ambapo wajumbe wake huchaguliwa na wanachama katika mkutano mkuu. 

Kamati ya Usimamizi

Kamati hii itakuwa na wajumbe watatu ambao watachaguliwa na Wanachama kwa ajili ya kuhakisha kuwa, taratibu za uendeshwaji wa Chama unazingatia Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 06 ya mwaka 2013 na Masharti ya Chama pamoja na miongozo mingine. 

Kamati ya Mikopo

Kamati hii itakuwa na wajumbe watatu ambao ni sehemu ya wajumbe wa bodi ambao huchaguliwa na bodi/mkutano mkuu. Kazi kuu ya kamati ya mikopo ni kusimamia utaratibu wa utoaji, ufuatiliaji na ufutaji wa mikopo kwa kuzingatia Sera ya Mikopo na Masharti ya Chama katika sharti dogo namba 55. 

Menejimenti ya Chama

Menejimenti ya Chama itakuwa chini ya Meneja, Chama kitaajiri au kuazima watumishi wenye ujuzi unaotakiwa katika kutekeleza kazi za Chama ambazo ni pamoja na:- 

a) Menejimenti na utawala. 

b) Uhasibu. 

c) Ukaguzi wa ndani. 

d) Kutoa na kufuatilia mikopo. 

e) Kazi za muda maalumu. 

f) Kazi nyingine (Watendaji wa kada za kawaida). 

Muundo wa Chama

Mchoro wa Muundo wa Chama