Historia ya Chama
Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Wafanyakazi NSSF Limited (NSSF EMPLOYEES SACCOS LTD) ni Taasisi ya huduma ndogo ya fedha iliyoanzishwa na Wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kuandikishwa na Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Dar es Salaam tarehe 11 Julai, 2001 kwa hati yenye usajili namba DSR. 2056
Fungamano la pamoja kwa Chama ni Wafanyakazi wa NSSF waliopo kazini, Wastaafu, wa NSSF, Watendaji ya Chama pamoja na wengine ambao watapata udhamini wa Wanachama hai watatu.
