NSSF EMPLOYEES SACCOS

NSSF EMPLOYEES SACCOS LTD

Dira na Dhima

Utangulizi

Mamlaka ya Chama yanatokana na Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya mwaka 2013 na Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha Na. 10 ya mwaka 2018 na Kanuni zake. Chama kilianzishwa ili kukuza maslahi ya kiuchumi ya wanachama kwa kuzingatia kanuni saba (7) za Ushirika ambazo ni:- 

a) Uanachama wa hiari na ulio wazi; 

b) Wanachama na Udhibiti wa Kidemokrasia; 

c) Ushiriki wa wanachama katika Shughuli za Kiuchumi; 

d) Uhuru na Kujitegemea; 

e) Elimu, mafunzo na taarifa; 

f) Ushirikiano miongoni mwa Vyama vya Ushirika; 

g) Kuijali Jamii.

 

DIRA

Kuwa SACCOS inayoongoza Tanzania kwa kutoa huduma bora ya mikopo kwa haraka na yenye masharti nafuu. 

Dhamira

Kukusanya Akiba na kutoa mikopo kwa wakati kukidhi matarajio ya wanachama kwa kutumia ubunifu, teknolojia ya kisasa na rasilimali watu mahiri. 

Misingi ya Chama

Misingi ni suala la muhimu wakati wa kusimamia shughuli za Chama kwani husaidia kufikia malengo ya Chama kwa wakati. Chama kitazingatia misingi ifuatayo wakati wa kutekeleza shughuli zake:- 

  1. Ushirikiano/Mshikamano(Solidarity) 

  2. Uwajibikaji (Self responsibility) 

  3. Kujali Wanachama 

  4. Uwazi (Transparency) 

  5. Ustadi 

  6. Uaminifu (Honesty) 

  7. Kujitolea na kujitegemea (Self help) 

  8. Uadilifu 

  9. Usawa (Equality) 

  10. Demokrasia 

Mwelekeo wa Chama

Thamani ya msingi ya kudumisha Chama imejengwa Katika Mihimili ya:- 

a) Uadilifu na Uaminifu; 

a) Kutoa huduma nzuri na zenye ufanisi kwa Wanachama; 

b) Kubuni, kuboresha na kuendeleza huduma na bidhaa bora kwa Wanachama; 

c) Umoja na ushirikiano; 

d) Haki na usawa katika kuwahudumia Wanachama; 

e) Kupiga vita rushwa; 

f) Kushiriki katika majukumu ya kijamii; 

g) Kutumia utaalamu katika uongozi na kufuata misingi ya utawala bora; 

h) Kuendesha Chama kwa misingi ya uwazi na uwajibikaji; 

i) Kuheshimu usawa wa kijinsia katika uongozi wa Chama.  

Malengo ya Chama

Malengo makuu ya Chama ni pamoja na:- 

i. Kuhamasisha uwekaji wa Akiba, Hisa na Amana ili kuendeleza na kukuza mtaji wa Chama. 

ii. Kutoa elimu kwa watumishi wa Chama ili kujua umuhimu wa kujiunga na Chama. 

iii. Kujengea uwezo Wanachama kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu ili kuwainua kiuchumi. 

iv. Kutoa elimu kwa Wanachama ihusuyo bidhaa za Chama. 

v. Kutafuta vyanzo nafuu vya fedha (mpango wa ukwasishaji) ili kujenga na kuimarisha mtaji wa ndani kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanachama kwa masharti na riba nafuu; 

vi. Kuweka viwango vya gawio katika hisa, faida juu ya Akiba na riba za Mikopo kwa Wanachama vinavyokidhi gharama za uendeshaji wa Chama; 

vii. Kubuni na kutoa bidhaa mbalimbali za fedha kwa Wanachama ili waweze kushiriki zaidi katika kuimarisha mtaji wa Chama na mitaji yao binafsi na kuleta mvuto kwa wasio Wanachama kujiunga na Chama.