NSSF EMPLOYEES SACCOS

NSSF EMPLOYEES SACCOS LTD

Kuhusu Sisi

Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Wafanyakazi NSSF Limited (NSSF EMPLOYEES SACCOS LTD) ni Taasisi ya huduma ndogo ya fedha iliyoanzishwa na Wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kuandikishwa na Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Dar es Salaam tarehe 11 Julai, 2001 kwa hati yenye usajili namba DSR. 2056.

Fungamano la pamoja kwa Chama ni Wafanyakazi wa NSSF waliopo kazini, Wastaafu, wa NSSF, Watendaji ya Chama pamoja na wengine ambao watapata udhamini wa Wanachama hai watatu.

Chama kinaendesha shughuli zake katika jiji la Dar es Salaam, Makao makuu ya Ofisi za Chama yapo katika Jengo la RITA TOWER ghorofa ya 13 mtaa wa makunganya na Simu, mkabara na jengo la Benjamin mkapa makao makuu ya NSSF. 

RITA TOWER
Rita Tower, Makao makuu ya NSSF Saccos

Muundo wa Uongozi wa Chama ina wajumbe wa Bodi saba (7) ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi na Makamu Mwenyekiti, Kamati ya Usimamizi yenye Wajumbe watatu (3) akiwemo Mwenyekiti na wajumbe wawili, Kamati ya Mikopo yenye Wajumbe watatu (3) na kwa sasa Chama kina Watendaji watatu (3). 

Mpango biashara huu umeandaliwa kwa kuzingatia ushirikishwaji wa Wajumbe wa Bodi, Kamati ya Usimamizi, watendaji, wanachama na wadau mbalimbali wa Chama. 

Njia zilizotumika katika uandaaji wa mpango biashara huu ni pamoja na kufanya thathmini ya ndani juu ya utoshelevu na ukamilifu wa utoaji wa huduma na taratibu zake, kuanisha changamoto za kiutendaji/uendeshaji na kutoa maoni juu ya nini kinapaswa kufanyika ikiwemo uanzishwaji wa mifumo thabiti ya TEHAMA na udhibiti wa ndani, uongozi na usimamizi, mfumo wa ukaguzi wa ndani pamoja na kuanzisha huduma tofauti za mikopo na bidhaa mbalimbali za akiba.